WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

BIRTHDAY YA MAMA YAKE DIAMOND AMZAWADIA GARI LA MILIONI 38

Ingawa Diamond hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mama yake. 
Ni Toyota Lexus New Model ambapo Babu Tale amesema imegaharimi milioni 38.1 ambapomilioni 35 imetumika kulinunulia gari hilo mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1 imetumika kulipamba na kuweka Music System pamoja na seat Cover.
Zawadi hii ameitoa Diamond kwa mama yake kama zawadi kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa mama yake ambaye amesema ametimiza miaka 55, mama yake amesema hakutegemea zawadi hii na anamuombea mwanae kwa Mungu afanikiwe zaidi.
                                                                                                      

Baada ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale alitangaza utaratibu wa kuzindua kwanza video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo hapo kisha utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha kukabidhiwa gari yake
 
                                                                                           

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Kiongozi wa maandamano Nigeria mbaroni

Shule hii ndio waliokuwepo wasichana hao waliotekwa
Mwanaharakati mwanamke aliyekuwa akiongoza maandamano nchini Nigeria kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuwaokoa wasichana 200 waliotekwa hivi karibuni ametiwa mbaroni na polisi kwa amri ya mke wa Rais wa nchi hiyo.
Naomi Mutah Nyadar alikuwa miongoni wanawake waliohudhuria mkutano ulioitishwa na ma mke wa rais Patience Jonathan na baadae mwanaharakati huyo alipelekwa kituo cha polisi habari zinasema.
Inasemekana Mke wa Rais Jonathan anahisi mama za wasichana waliotekwa walimtuma mwanaharakati huyo ili aweze kuwawakilisha.
Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Mchambuzi wa masuala ya Nigeria anasema Mke wa Rais Jonathan ni Mwanasiasa mwenye nguvu nchini Nigeria.
Mama Mutah mwakilishi wa jamii ya Chibok eneo ambalo wasichana hao walipotekwa wakiwa shuleni zaidi wiki mbili zilizopita, wiki iliyopita aliandaa maandamano katika mji mkuu wa Abuja.
Waandamanaji wengi wakiwa ni Wanaigeria wanaona serikali ya nchi hiyo haijafanya vya kutosha kuwatafuta wasichana hao waliotekwa wanaodhaniwa kuwa ni kundi la kiislam la Boko Haram.
Hadi sasa Boko haram hawajasema lolote kuhusu tuhuma hizo.
 Wasichana wanne walio mbele ambao ni miongoni mwa waliotekwa na kufanikiwa kutoroka



  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
Kundi la kislamu nchini Nigeria la Boko Haram linasema kuwa ndilo lililowateka nyara zaidi ya wasichana wa shule 200 ambao hawajulikani waliko kwa wiki tatu sasa.
Kupitia kwa njia ya video kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau amesema kuwa watawauza wasichana hao. Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi.
Wasichana hao walitekwa kutoka katika shule moja kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Wakati huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa ameshikiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais wa nchi hiyo Patience Jonathan amechiwa huru.
Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao.
Akizunguma kwa mara kwa kwaza rais wa Nigeria Goodluk Jonathan amesema kuwa atafanya awezalo kuwakoa wasichana hao.
 

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

WASTARA JUMA NDIO MCHEZA FILAMU WA KIKE BONGO MWENYE USHAWISHI KAMA KIONGOZI

Hii inatokana na jinsi anavyojituma kwenye kazi zake za sanaa na kuwa karibu na mashabiki wake jambo linalofanya azidi kupendwa kila kukicha
Wakipiga stori baadhi ya mashabiki wake wanasema Wastara ni msanii anaeipenda kazi yake na sio mbaguzi wala hana majivuno yani ni mtu wawaatu
“Unajua wastara ni tofauti na wasanii wengine yani pamoja nakua kwenye game kwa miaka mingi bado ashuki samani kila msanii anatamani kufanya nae kazi“

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

ILIZOPITA. HUYU NDO MKE WA NAPE NNAUYE WALIYEFUNGA NAE NDOA SIKU CHACHE ZILIZOPITA.

https://fbcdn-sphotos-c-a.akamaihd.net/hphotos-ak-frc1/t1/1891079_690906487640003_1909330052_n.jpg
Wakati wa Kufunga Ndoa

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

KESI YA MGANGA WA KIENYEJI DHIDI YA AT YASOMWA LEO

Ile kesi inayomkabili mwanamuziki wa miondoko ya Miduara Ally Ramadhani maarufu kama AT dhidi ya Mganga wa kienyeji leo ndio ilikuwa tarehe yake ya kusomwa katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni jijini Dar es Salaam  
AT alifika mahakamani mapema Asubuhi leo hii na ilipofika zamu ya kusomwa , Aliingia mahakamani na kusomewa mashtaka yake lakini kesi hiyo imepigwa Tarehe mpaka 2 April 2014 
Ambapo Mdai Dr Sharif anatakiwa kwenda na vilelezo vinavyothibitisha madai hayo
Dr Sharif anadai kati ya mwaka 2010 mpaka 2013 alimtibia Msanii huyo na humlipa
Matibabu hayo ni pamoja na kuinua Nyota na kusaidia kumpa Tunzo mwaka
2013

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

UTAJIRI WA DIDA WA TIMES FM WAZUA GUMZO DAR ES SALAAM

AMINI usiamini lakini ndivyo ilivyo! Utajiri wa Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ umeibua gumzo midomoni mwa watu wakidai kuna walakini juu ya upatikanaji wake

Toyota verossa ikiwa imepaki katika gholofa analodaiwa kumiliki Dida

 Magari aina ya Toyota Verossa yakiwa yamepaki katika sehemu maalumu ambayo anamiliki  Dida
MAGARI MATANO YA KUTEMBELEA

Chanzo chetu kikazidi kwenda mbele kwa kudai kuwa mbali na umiliki wa nyumba, pia mwanadada huyo ana magari matano kwa ajili ya kutembelea tu.
“Mbali na nyumba hizo, Dida pia ana magari matano ambayo hubadili anavyotaka kwa ajili ya kutembelea tu kwenye mizunguko yake.

“Ana Toyota Verossa mbili, ana Toyota Noah rangi ya silva na nyeusi. Ana Toyota Vitz. Hivi karibuni ameanza mchakato wa kuingiza nchini gari lingine la sita aina ya Range Rover ‘Vogue’. Hebu fikirieni, Dida huyuhuyu mnayemjua, amepata wapi mali hizo?” kilihoji chanzo.
 Maduka matatu yanguo anayo miliki Dida yaliyo katika viiwango vya juu ambayo yapo Dar es salaam Na katika Mabango ya maduka hayo yanasomeka Dida Classic ambayo yapo kinondon ya nguo za kike
MISUKO SUKO YA NYUMA ALIOWAHI KUPATA DIDA
kabla ya kudaiwa kuwa na utajiri huo,Dida alikumbana na misukosuko ya madeni Benki moja jijini ilidaiwa kufilisi Thamani za nyumbani kwake kinondoni jijini Dar es salaam baada ya kuushindwa kulipa mkopo
DIDA AUNGELEA UTAJIRI WAKE
watu wamekuwa wakiongelea sana kuwa nauza unga kitu ambacho si kweli na hakina ukweli wowote ndani yake kwanza hata siujui huo unga na fananaje ukweli ni kwamba mimi najituma katika kazi na kufanya biiashara aligusia kuwa hatosahau siku ambayo watu wamekwwenda kutoa taarifa uwanja wa ndege JK nyerere Airport kuwa siku hiyo alikuwa anasairi  na mzigo wa madawa ya kulevya
Alipoika Airport Dar es Salaam aliwekwa chini ya ulinzi na kupekuliwa kila alichokuwa amebeba haikutosha alipelekwa katika Hospital ya Temeke Dar na kuufanyiwa X-ray na hawakuona kitu nilirejea Airport na kuendelea na safari
mimi nawacha waongee tu kwani hawajui ninachokifanya kwani mimi najitambua na kile ninachokifanya pia
Toyota Vitz kama ya Dida 
kuhusu toyota vitz amesema anampango wa kuingiza nchini na mda si mrefu atakuwa amekamilisha kwani hafuatilii maneno yanayosemwa kwamba wote waliopeleka tarifa airport hawana lolote ila ni wivu tu 
   

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

KICK MPYA ANAYO ITAFUTA USTADHI JUMA NA MUSOMA KUPITIA ACCOUNT YAKE YA INSTAGRAM

 Ustadhi akiwa  katika pozi pix alizopost kupitia Account yake

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

WOLPER ACHOMOA SKENDO YA KUTELEKEZA WAZAZI

Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amechomoa madai yaliyoibuka kuwa hawajali wazazi wake.Baada ya taarifa hizo za chinichini kuzagaa, Wolper aliibuka na kuzikanusha:
“Wazazi wangu ni matajiri kwa pesa gani nyingi nilizonazo za uwafikia wao kiasi cha kuwapa matunzo, bado nawategemea hivyo wanaodai nimetelekeza wazazi ni waongo tu.”

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

FLORA LYMO AMWAGIA SIFA KEDE KEDE MANGE KIMAMBI

Flora Lymo ameamua kufunguka kwenye Blog yake kuhusu Mange Kimambi na Haya ndio Aliyoandika:

"Mama na Mwana'' Yani hii ndiyo sababu sana sana nikamuweka Mange kwenye hii Blog yenu ya maukweli matupu leo'Flora Lyimo Fashion Police Blog' Yani Im so PROUD of you Mange'' kwa kuweza kutokumkataa mwanao kwa sababu umeolewa na Mzungu au Mwanaume Mwengine wa aina yoyote aliekukuta wewe ukiwa na Mwanao au wanao ''yani Wanawake /Dada wengi huwakataa watoto wao kisa ni wamempata Mzungu au Mme wa kuwaowa'' Why do that jamani ?''Just take a look at Mange hapa na mwanae wanavyopendezeana yani is the Best think you can ever do to your Child'' Love them hata kama umempata Mme wa dhahabu au Gold'' Please Igeni Mfano wa Mange hapa'' Be Bless Mange na familia yako '' Yani huwa ni lazima ukiwa unakizuri ninachokijua Moyoni mwangu nitakisema na vile vile kibaya'' hiyo ndiyo habari ya mujini always say the truth''

Sasa hebu ona Jamani wanavyopendeeana ,alafu wewe uwe umemkana mwanao unajilia maraha yako mwenyewe na tena bila hata haya unazaa na watoto wengine na huku ukiwakataa wanao wengine''yani wenyewe tabia hizo wacheni mara moja please'' is not nice ,just take a look of hii Familia ya our Star Mange Kimambi na Familia yake''so lovely ''Yani naona aisee hata Mimi my Birthday mwaka huu niifanye hivi ''Just me and my Family ''wacha nijipange fasta fasta maana yakaribiaaaaaa''Ruwa Mangi'' Anyway''Hope nyie mnao wakana watoto wenu mnaisoma hii na kumuiga Mange Kimambi hapa''
Again Happy Birtday and wishing you All the Best utuzalie Mtoto wetu salama''

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

ACCOUNT FAKE YA FACEBOOK YA KALA JAREMIAH YAZIDI KUDHALILISHA WANAMUZIKI SASA ZAMU YA LADY JAY DEE


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Magari ya umma yavuruga shughuli Nairobi

Wahudumu wa magari ya umma wakigoma Nairobi

Jiji la Nairobi ni mojawapo wa kaunti ambazo zimebuniwa chini ya Katiba iliyopitishwa na wapiga kura na kuidhinishwa mwaka 2010 katika hatua ya kuimarisha huduma kwa wananchi.

Kaunti hizo mpya hata hivyo zimejikuta njia panda baada ya kupata madaraka bila fedha za kuandamana nayo; ambapo zimelazimika kuongeza kodi kama njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi.

Mkuu wa polisi nchini Kenya, David Kimaiya aliagiza idara ya trafiki nchini Kenya kunasa magari yote yaliyofunga barabara za mji.


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Mapigano mapya mjini Juba

Wanajeshi wa waasi nchini Sudan Kusini

Wanajeshi watano wa serikali ya Sudan Kusini wameuawa kufuatia mapigano makali ndani ya kambi moja ya kijeshi mjini Juba.

msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema kuwa wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye mapigano hayo iliyotokea katika kambi ya jeshi ya Jebel.

Mapigano kama hayo ndani ya kambi hiyo kati ya makundi hasimu yalisababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Mkaazi mmoja wa Juba ameiambia BBC, kwamba moshi mweusi ulionekana ukitapakaa angani juu ya kambi hiyo karibu na chuo kikuu cha Juba na kwamba watu wameonekana wakilitoroka eneo hilo.

Akiongea muda mfupi kwenye runinga ya taifa muda mfupi baada ya mapigano hayo kuanza, Brigadier General Malak Ayuen Ajok amesema kuwa waliouwa ni wanajeshi waatiifu kwa serikali.

Amesema mapigano hayo yalisababisha na mvutano kati ya wanajeshi ambao walikuwa wakizozana kuhusu kucheleweshwa kwa mishahara yao.

Ajok, ameongeza kuwa hakuna dalili yoyote ya mapigano hayo kusambaa katika maeneo mengine ya mji huo.

Lakini watu wengi wanaoishi karibu na kambi hiyo ya wamekimbia makwao na kutafuta hifadhi katika piga makanisa na shule.

Mzozo wa Sudan kusini ulianza mjini Juba, mnamo mwezi Disemba mwaka uliopita kufuatia hali ya wasiwasi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar lakini ukaenea kote nchini humo.


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

BABY MADAHA AFUNGUKA "SHILOLE NI MCHEZA VIGODORO"

MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Madaha’ amemchana staa mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumwambia ni mcheza muziki wa uswahilini (vigodoro).

Kauli hiyo ya msanii huyo anayetamba na Wimbo wa Summer Holyday, ameitoa siku chache baada Shilole kutema cheche zake kuwa Madaha aache kumfuatilia kwani amekuwa akiingia kwenye anga zake mara kwa mara.

“Hivi huyu ana akili au matope, nimfuatefuate ana nini? Hebu aangalie muziki wangu ninaopiga na wake. Yeye ni wa hapa hapa, mcheza vigodoro,” alifunguka Madaha

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

TAARIFA KUHUSU KUACHISHWA KAZI KWA KOCHA WA TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

MWEE ETI MIMBA YA LINAH YACHOROPOKA

SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka.

Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.

“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu.

Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.

“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.
Credits:GPL

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

ALI KIBA AELEZEA SABABU ZA UKIMYA WAKE KWENYE GAME YA MUSIC

Kwa kipindi kirefu mkali wa ‘Single Boy’ Ali Kiba amekuwa kimya bila kutoa kazi yake binafsi huku ukimya wake ukizua maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa muziki Tanzania.
Lakini leo (February 25) Ali Kiba amezua maswali mengine kwa mashabiki wake baada ya kuweka kwenye Instagram picha inayomuonesha akiwa na AY na Mwana Fa na kuandika ‘@Aytanzania&007#mj record #wait for it bonge ya wimbo.’

Hata hivyo hakuweka wazi kama ni wimbo wake au ameshirikishwa na maswaiba hao.

Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano na Ali Kiba ambaye ameyajibu maswali hayo yote, maswali ambayo hapo awali yalikuwa na majibu ya kuhisia tu bila kuwa na uhakika.

Ali Kiba ameiambia tovuti hii kuwa aliweka picha hiyo kwenye Instagram lakini hakuweka maelezo ya kutosha kwa makusudi.

“Sababu ya kuweka vile ni katika kutaka tu kuwa-surprise watu kwa sababu sikupenda kuwambia ni ngoma ya nani ila nimewajulisha kuwa nimefanya nao na tumefanya kwa MJ, hiyo yote ni kutaka kuwa-surprise.” Amesema Ali Kiba.

Mwimbaji huyo amedai kuwa hadi sasa wimbo huo haujajulikana ni wa nani kati yake yeye, Mwana Fa na AY, “tumefanya wote…haijajulikana ngoma ni ya nani.”

Ali Kiba ameongeza kuwa mashabiki wampe miezi miwili ijayo na kisha watapata maelezo ya kutosha kutoka kwake na kwamba baada ya muda huo kila kitu kitakuwa sawa.

Mwimbaji huyo wa ‘My Everything’ ameeleza pia sababu za yeye kuwa kimya, pamoja na mpango wake kwa mwaka 2014 ambapo amedai kuwa ataachia albam yake mpya.

“Sababu ya kuwa kimya ni kumpush Abdu Kiba aweze kuwa sawa sawa na vilevile mimi ni mzazi kwa hiyo niko busy na jinsi ya kuwa baba. Yaani vitu vingi vyote nilikuwa nikifanya, wakati muda wote niliokuwa nikifanya hivyo vitu nilikuwa najiandaa na albam yangu nyingine ambayo ni ujio mpya…nakuja na everything.

“Albam ipo kwa sababu itakuwa chini ya usimamizi wa kampuni ambayo inanihost, na ndio maana nikakwambia nipe miezi miwili na watu watajua kila kitu kinachoendelea…itafanyika na usimamizi mzuri tu na process zote zitakuwa ziko okay. Ila siwezi kukwambia ntafanya na distributor gani lakini, wasimamizi wangu watafanya hilo, wasimamizi ambao wamenichukua ndio maana ukaona kimya kingi, ni ku-fight maandalizi na kumaliza ngoma.”

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Mabomu yaripua hoteli mbili Mogadishu

Mogadishu, Somalia
Polisi nchini Somalia wanasema mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu yameuwa watu kama 15.
Polisi walieleza kuwa mabomu hayo yaliripuka kwenye mkahawa uitwao The Village ambao unapendwa na waandishi wa habari na maafisa wa vikosi vya usalama, pamoja na hoteli Muna, ambako wabunge wengi hukaa.
Hoteli zote mbili ziko karibu na ikulu ya rais.
Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulio hayo, lakini hoteli zote mbili zimewahi kushambuliwa na wapiganaji wa Kiislamu, al Shabab.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Wasichana watakiwa kuvaa makoti India

Maandamano dhidi ya ubakaji India
Chama cha upinzani cha India, BJP, kimeiomba serikali ya mji wa Pondicherry, kusini mwa nchi, kuwapatia watoto wa shule makoti wavae ili wasinyanyaswe kijinsia. Katibu wa chama alitoa taarifa kusema kuwa unyanyasaji ni tatizo hasa katika shule za serikali, na kwamba wasichana wote wapewe makoti na piya wapate fursa ya kueleza malalamiko yao bila ya kujitambulisha.
Visa vya ubakaji vimezidi kuripotiwa nchini India na kupelekea sheria mpya kupitishwa.
Lakini baadhi ya viongozi wamelaumiwa kwa kutazama maisha ya wanawake tu, badala ya kubadilisha tabia za wanaume.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Polisi waondoka medani ya Taksim

Maandamano katika medani Taksim, Istanbul
Baada ya mapambano ya siku mbili na waandamanaji, polisi wameondoka katika medani ya Taksim mjini Istanbul na maelfu ya waandamanaji wameikalia medani hiyo.

Hapo awali waziri mkuu wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan, alitoa wito watu waache kuandamana haraka - maandamano makubwa kabisa kwa miaka kadha.
Lakini Bwana Erdogan ameahidi kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba polisi walitumia nguvu nyingi.
Nchi kadha zimeeleza wasiwasi kuhusu swala hilo.
Chanzo cha maandamano ni mpango wa kujenga maduka katika medani ya Taksim - mpango ambao Bwana Erdogan anasema atautekeleza.
Waandamanaji vijana piya wanailaumu serikali kwamba imekuwa ya kimabavu na kuifanya nchi kufuata Uislamu.
Msemaji wa serikali alikanusha malalamiko hayo alipohojiwa na BBC na alisema tuhuma zenyewe ni za kushangaza.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Urusi yazinga azimio kuhusu Qusair

Mwanaharakati wa Qusair akitembea katika mji huo unaoshambuliwa na jeshi la serikali ya Rais Assad
Wanabalozi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanasema kuwa Urusi imezinga mswada wa azimio la kueleza wasiwasi kuhusu hali, hasa ya raia, kwenye mji wa Syria wa Qusair ambao umezingirwa.

Mashambulio ya serikali dhidi ya mji huo unaodhibitiwa na wapiganaji yameendelea kwa zaidi ya majuma mawili na wakaazi wamenasa bila ya chakula, maji wala madawa.
Lakini wanabalozi wanasema Urusi haitaunga mkono mswada huo wa azimio kwa sababu Umoja wa Mataifa haukushughulika wakati mji huo ulipotekwa na wapiganaji.
Hapo jana Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, yalitoa maombi kuwa wasaidizi waruhusiwe kuingia Qusair.
Msemaji wa ICRC, Dibeh Fakhir, aliiambia BBC taarifa wanazopata kuhusu hali katika mji huo:
" Ripoti tunazopata zinasema kuna upungufu mkubwa wa maji, chakula na madawa.
Piya zinaeleza kuwa mamia ya raia wamejeruhiwa na hawawezi kupata matibabu.
Maelfu tayari wameshakimbia Qusair na maelfu wanasaidiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Syria, likisaidiwa na ICRC na mashirika mengine.
Hata hivo inaripotiwa maelfu bado wako ndani ya mji - kati yao ni mamia waliojeruhiwa vibaya lakini haiwezekani kuwatibu"
Alisema kuweza kusaidia inavyotakiwa, ICRC inahitaji kuwepo Qusair bila ya kuingiliwa kati na serikali.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

sherta kuanzisha kampuni ya kusaidiakuinuwa wasanii wachanga


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Roma Juu ya Stage

Roma mkatoliki ndani ya viwanja vya Coco Beach Dar Es salaam Tamasha lilioandaliwa na Tigo

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

MATUKIO YA KUTISHA MWAKA 2012

moja ya maeneo jangwani
Mafuriko dar na kusababisha watu kukosa makazi maeneo ya Jangwani hadi maeneo ya kigogo Dar es Salaam
Milipuko ya mabomu yaliotokea mbagala na hatimaye gongolamboto hivyo hatuta sahau kamwe swala hili jamani ndugu zetu walipoteza makazi na wengine kupotezana kwa milipuko iliotokea katika kambi ya jeshi gongo lamboto
Walimu wa msingi waligoma kwa kudai huenda ni haki yao kudai kwa kudai vitu kuwa juu na kusababisha ndugu zetu watoto wetu kukosa masomo kwa siku husika
Mgomo mkubwa ulioleta athari nyingi kwa wagonjwa na kufanya matibabu kusimama kwa tuhuma juu ya mishahala na posho za madaktari muhimbili wagonjwa walipata tabu sana kulingana na mgomo huo
Hatuta sahau mwaka 2012 vurugu za kariakoo zilizosababishwa na vikunndi vinavyosemekana kuwa ni vya kidini vilivyosababisha hadi jeshi la wananchi kuingilia kati na vikundi vya kutuliza ghasia kuingilia ili kuweka amani maeneo ya kariakoo wengi waliumia na kupata ulemavu
vifo vingi vilivyotokea mwaka 2012 zanzibar kwa kuzamakwa meli na kusababisha watu wengi kupoteza maisha
Hatuta sahau vifo vya wasaniii vilivyotokea mwaka huu ikiwemo Steven Charles Kanumba , Hussein Ramadhani Nkieti , Mlopelo na wengineo taifa litawakumbuka kwa yale mlioyafanya mungu amilaze mahala pemapeponi amini
Hatutasahau vurugu zilizotokea Zanzibar zilizosababishwa na kundi la muamsho na kusababisha mali za watu kupotea na wengine kupoteza maisha  Mungu atulinde atupe amani Mwaka 2013


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

SHIDA YA MAJI YAZIDI WILAYANI MUHEZA TANGA

Bado wilaya ya muheza shida ya maji imezidi kjuwa kubwa zaidi japo kjuwa jitihada za viongozi zinaendelea na jitihada za utatuzi wa tatizo hilo lakini bado wakazi wa wilaya hiyo wanapata tabu sana na shida ya maji ,jitihada ambazo zinafanywa na manispaa nzima ya wilaya hiyo ni kutoa maji katika mto zig na kusamabaza katika wilaya nzima japo kuwa bado mpango huo haujakamilika

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS