Chama cha upinzani cha India, BJP, kimeiomba serikali
ya mji wa Pondicherry, kusini mwa nchi, kuwapatia watoto wa shule
makoti wavae ili wasinyanyaswe kijinsia.
Katibu wa chama alitoa taarifa kusema kuwa
unyanyasaji ni tatizo hasa katika shule za serikali, na kwamba wasichana
wote wapewe makoti na piya wapate fursa ya kueleza malalamiko yao bila
ya kujitambulisha. Visa vya ubakaji vimezidi kuripotiwa nchini India na kupelekea sheria mpya kupitishwa. Lakini baadhi ya viongozi wamelaumiwa kwa kutazama maisha ya wanawake tu, badala ya kubadilisha tabia za wanaume. |
Wasichana watakiwa kuvaa makoti India
Posted by
RAMADHANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment