Kundi la kislamu nchini Nigeria
la Boko Haram linasema kuwa ndilo lililowateka nyara zaidi ya wasichana
wa shule 200 ambao hawajulikani waliko kwa wiki tatu sasa.
Kupitia kwa njia ya video kiongozi wa kundi hilo
Abubakar Shekau amesema kuwa watawauza wasichana hao. Wasichana hao
walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi.Wakati huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa ameshikiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais wa nchi hiyo Patience Jonathan amechiwa huru. Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao. Akizunguma kwa mara kwa kwaza rais wa Nigeria Goodluk Jonathan amesema kuwa atafanya awezalo kuwakoa wasichana hao. |
Posted by
RAMADHANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment