WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Baadhi ya Mali zilizopotea Katika Ajali ya Sharo zapatikana ila pesa Bado

Mpaka sasa inasemekana kuna baadhi ya mali za Marehemu Sharo milionea zimepatikana na zipo kituo cha polisi mali hizo ni simu lakini bado pesa zilizopotea wakati wa ajali ya msanii Huyo iliosabababisha kifo chake papo hapo katika maeneo ya maguzoni wailayani muheaza Mkoanai tanga lakini bado jeshi la polisi linaendelea na upelelezi juu ya upatikanaji wa fedha hizo mali ambazo zinasemekana zimepatikana ni pamoja na simu za marehemu pamoja na Radio ya gari pongezi za dhati zinhitajika kaitika kupewa jeshi la polisi kwa jitihada zao na endapo tunaomaba endapo watapatika na Sheria ichukuwe mkondo wake kwani hwana hata huruma watu hao tena wakamatwe

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Uingereza yasitisha msaada kwa Rwanda

Wananchi wakitoroka mapigano
Uingereza imesitisha kwa muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa nchi hiyo katika mzozo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mawaziri walisema kwamba Uingereza sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21.
Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba, hata baada ya tashwishi kuwepo kuhusu tetesi kwamba ilikuwa inawaunga mkono wanamgambo wa M23 wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali ya Uingereza ilikuwa imesema kwamba ingetoa kitita kingine cha pauni milioni 18 kwa ajili ya mahitaji ya kibandamu ya dharura huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Makubaliano
Sasa fedha hizo, ambazo zilikuwa zitolewe mwezi ujao, hazitatolewa tena kwa sababu serikali ya Rais Paul Kagame imekiuka makubaliano.
Nyaraka ya Umoja wa Mataifa iliyofichuliwa inasema kwamba waziri wa ulinzi wa Rwanda ndiye anayewaamrisha waasi walioko huko.
Mapigano hayo yamepingwa na nchi za kimataifa, huku Marekani na nchi kadhaa za Ulaya zikizuia msaada uliokuwa umepangwa kwa ajili ya Rwanda.
Waziri Justine Greening wa Uingereza alisema: “Nimeamua kutotoa fedha zilizokuwa zimekusidiwa kwa ajili ya kuisaidia bajeti ya Rwanda. Ni wajibu wetu kujaribu kutafuta suluhu za kudumu kwa mzozo wa eneo hili, na kufanya kazi pamoja na serikali za Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kuhakikisha suluhisho la amani linapatikana mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo."

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Rasimu ya katiba Misri yaidhinishwa

Generali Mamdou Shahin (Kulia) akishauriana na maafisa wa kamati ya katiba kabla ya kupigiwa kura
Kamati inayoandika katiba nchini Misri imeidhinisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Hayo yaliafikiwa katika shughuli iliyochukua saa kumi na sita, na kamati hiyo ilikubaliana kwa kauli moja kupitisha vifungu viwili thelathini na nne.
Rasimu hiyo sasa sharti iidhinishwe na rais Morsi kabla ya kupigiwa kura ya maoni.
Wanasiasa waliberali pamoja na wakristu walisusia shughuli za kamati wakisema walihisi kutengwa.
Akizungumza kwa runinga awali Rais Mohamed Morsi amesema kuwa atajiondolea mamlaka mapya aliyojikabidhi pindi tu watu watakapokubaliana kuhusu katiba.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

HESHIMA NA SWALAA YA MWISHO KWA SHARO MILIONEA

Mwili wa Marehemu Sharo milionea ukiswaliwa kwa mara ya mwisho na watu waliofika msibani nyumbani kwao Katika kijiji cha Lusanga Muheheza tanaga

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

MZEE MAJUTO RAFIKI WA KARIBU SANA NA MAREHEMU SHARO MILIONEA AKIELEKEA MAKABURINI

Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea mazishini kuupumzisha mwili wa marehemu Sharo milionea mazishi yalifanyika nyum,bani kwao Mkoani Tanga katika kijiji cha Lusanga wilayani Muheza mazushi hayo yalihudhuriwa na watu wa aina tofauti tofauti kulingana na wanavyomfahamu sharo milionea kwa kazi zake alizokuwa akifanya kipindi cha  uhai wake na kunawasainii wengi walioguswa na msiba huo pia walihusika katika mazioshi munguailaze roho ya marehemu mahala pema peponi

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

200 wajeruhiwa wakitafuta kazi Tunisia

Mmoja wa waliojeruhiwa wakitafuta ajira huko Tunisia
Zaidi ya watu mia mbili walijeruhiwa huko Tunisia Jumatano katika siku ya pili ya maandamano jijini Siliana kilomita mia moja Ishirini kutoka katika jiji kuu la Tunis.
Waandamanaji hao walikuwa wakimtaka gavana wa eneo hilo kujiuzulu, kutaka msaada wa kiuchumi na vile vile kushinikiza watu kumi na wanne waliokamatwa katika ghasia za Aprili kuachiliwa.
Maafisa wa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kuwatwanya watu waliokuwa wanataka ajira. Pia kulikuwa na ripoti za watu kutibiwa baada ya kupata majeraha ya risasi.
Vyama vya wafanyakazi vimeitisha maandamano zaidi baadaye leo.
Tunisia ndiyo ilikuwa kitovu cha mapinduzi ya kiraia katika nchi za Kiarabu ambapo wananchi walimng'oa mamlakani rais wao wa muda mrefu Januari mwaka 2011.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

UN yasaidia Mali ingawa kwa tahadhari

Waasi wa Tuareg nchini Mali
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon ameunga mkono mapendekezo ya Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuidhinisha vikosi vya usalama vya kulinda amani vya AU vipelekwe Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisalamu Kaskazini ya Mali.
Hata hivyo ilikataa kutoa ufadhili wa Umoja wa Matifa katika shughuli hiyo.
Alionya kuwa kuingiliwa kijeshi katika eneo hilo kutasababisha hatari kubwa za kibinadamu na akataka kuwe na mipango ya kutuliza hali hiyo.
Wanadiplomasia wanasema kuwa vikosi hivyo vitatumia nguvu kupita kiasi ilihali vinatakiwa tu kutoa huduma za kusitisha vita kwa njia ya amani.
Hata hivyo bwana Bana hakutoa msaada wa kifedha na ksuema kuwa mataifa ya Afrika yanahitaji maswali kuhusu jeshi hilo litakavyoendesha kazi zake.
Viongozi wa Afrika wamekuwa wakitaka kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuunda jeshi la pamoja na nchi za Afrika Magharibi litakalosaidia jeshi la Mali kupambana na waasi.
Jeshi la Mali lilipoteza udhibiti wa Kaskazini mwa nchi ambalo linashikiliwa tena.
Kuhusu mapendekezo yake kwa baraza la usalama la umoja huo, bwana Ban alisema ataidhinisha wanachama wa muungano wa Afrika kuunda kikosi cha wanajeshi 3,300 ambao watajulikana kaa AFISMA kuweza kushika doria nchini humo kwa mwaka mmoja.
Alisema wataisaidia jeshi la Mali kurejesha hali ya utulivu kaskazini mwa nchi na kupunguza tisho la makundi ya kigaidi kuvamia eneo hilo

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Hali ya mzee majuto

Add captionAdd capti
YANAYOJIRI KWENYE MSIBA WA SHARO MILLIONEA:

Hali ya mzee King Majuto presha imepanda na hali kuzidi kuwa mbaya kutokana na kupata taarifa za msiba wa Sharo Milionea.

Mjomba wa marehemu Sharo Millionea, Bwana Omary Fundikira asema marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho, Jumatano. Hii ni kutokana na msanii mwenzake John Maganga kuzikwa leo.
...

Mkuu wa polisi mkoa wa Tanga RPC Costantine Massawe asema Hussein Ramadhani (Sharo Milionea) alikuwa mwenyewe katika gari na ilipotokea ajali gari lilimrusha nje na kufariki hapohapo.

Pia rafiki wa marehemu bwana Mohamed Ismail ambaye ndiye aliyemuazimisha gari alilopata nalo ajali, asema ilitakiwa waongozane kwenda Tanga pamoja ila alishindwa maana alipata majukumu mengine.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

TUTAKUKUMBUKA SHAROMILIONEA

Daima tutakukumbuka Broo kwa ubunifu wako mzuri tulikupenda lakini mungu ameklupenda zaidi pumzika kwa amani Sharomilionea  kilichobaki watanzania inatubidi tumrudie mungu kwani atujui lini itakuwa hatima ya maisha yetu sisi tunapanga hivi mungu nae anapanga vyake hatuna budi kumtukua kwa kila jambao ambalo llinatokea kwa kupitia kwake Ni wakati sasa wasanii kwa ujumla kuliangalia hili kwa umakini tukirudisha fikra zetu nyuma wangapi wamepita na walikuwa na umaarufu gani jee mimi na wewe tumejipanga vipi juu ya hiyo safari ambayo hatuijui muda , siku wala saa jamani tuliangalie hili kwa umakini na kiukweli kwa mwaka huu tumepata mapigo makubwa sana katika tasnia ya sanaa nchini hatutakaa tuhusahau mwaka huu kamwe jamni wasanii inabidi wawe na umoja katika kushiriki msiba huu bila kujali chochote

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Marehemu John Stephano Maganga, wakati wa uhai wake.


Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya, ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, ameelezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.
Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha anaendelea na kusema siku ya pili yake John alimpigia simu na kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii vizuri, kuona hivyo, baba yake mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta amelala kwenye kochi anatoka jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?, John akamjibu, tumbo linamuuma sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake mzazi nimwambie tumpeleke Hospital Mwananyamala.
Tulipofika pale hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari wakaamua wampige X Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu makali sana tumboni mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari, wakasema ana matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji wa haraka.
Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura (emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.
Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi nilifika Muhimbili na kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku wa jana yake. Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha kinachoendelea. Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu yule daktari ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani anamshughulikia hivyo alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza punguza makali ya sumu iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip ya maji lakini inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.
Muda mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena, amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake. Mazishi yamepangwa kufanyika makaburi ya kinondoni kesho. Alisema baba mdogo wa muigizaji Stephano.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

LUTENI KALAMA ASAKWA AULIWE NA KIGOGO WA SERIKALI!

Mwanamuziki wa siku nyingi kwenye game hiyo ya bongo flava,Luteni Kalama kuna madai anatafutwa na na mume wa Miss Ruvuma ambae amezaa nae mtoto mmoja ili amuue kwa risasi.
Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibuni na mwanamuziki huyo zilisema kuwa Luteni Kalama amekuwa na kwenye mahusiano ya kimapenzi na Miss huyo wakati ni mchumba wa mtu ambae ni kigogo mmoja anaefanya kazi Wizara ya Ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Nzenzely.
Chanzo chetu kilieleza  kuwa Issabaelah na Luten wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi kirefu ingawa wali walikuwa wamefanya kama siri lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda mambo yakawa hadharani hadi kigogo huyo kushtukia ishu.Hata hivyo kufuatia tuhuma hizo mwandishi wetu alimtafuta Kalama mwenyewe ili athibitishe sakata hilo ambapo alipataikana na kuizungumzia ishu hiyo kwa ujumla" Ni kweli na mimi nasikia kwamba natafutwa ili nipigwe risasi kwa vile nina ukaribu na Bellah,Lakini mimi namuachia mungu ingawa nina mpango wa kwenda kutoa taarifa Polisi" Alisema Kalama 
Aidha alipotafutwa mrembo huyo ili nae kuzungumzia alisema alikuwa na ya kusema"Hizo habari za kutafutana kwa bunduki mi hazini husu ukaribu wangu na Kalama ni wa kisanii na si vinginevyo" Alijibu kwa ufupi Miss huyo

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Ommy Dimpoz Poz Kwa Poz kuachia ngoma mpya

Ommy Dimpoz kuachia ngoma mpya week ijayo

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

TAKUKURU FUATILIENI FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI HALMASHAURI-GALLAWA

MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi ya kufuatilia fedha zinazopelekwa na serikali katika halmashauri nchini ili ziweze kutumika vizuri kwenye miradi mikubwa ysa maendeleo iliyokusudiwa.

Akifunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa takukuru kwenye hoteli ya Tanga beach Resort kwa maofisa wa taaisis hiyo kutoka mikoa yote ya tanzania bara, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa takukuru wamebeba dhamana kubwa ya kustawisha maendeleo kwa kufautilia watendaji kwenye halmasauri ambao wanatumia vibaya fedha zinazoolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.

Amesema serikali hasa ya awamu ya nne, imekuwa ikitoa fedha nyingi katika halmashauri kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maeneleo hasa ya elimu, afya, barabara na kujenga majengo mbalimbali lakini fedha hizo wakati mwingine zimekuwa zikitumika visivyo na hivyo kuleta malalamiko kutoka kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuipongeza taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuokoa fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni 97.5, lakini ameitaka takukuru kuhakikisha inaongeza kasi ya mapambano ya rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.

Kuhusu wananchi mkuu huyo wa mkoa amewataka kutoa ushirikiano kwa taaisis hiyo na waache kulalamikia masuala ya ufisadi wakati kama watatoa ushirikiano masula hayo yanaweza kudhibitiwa kwa watu kuogopa fedha za umma hatua ambayo mwelekeo wa taasisi hiyo inakoelekea na kwamba waongeze jitihada kutumia nyenzo walizokuwa nazo katika mapambano hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la mapambano ya rushwa ikiwemo kuwafundisha watumishi wake kwenda sambamba na mabadiliko ya teklonojia katika masuala ya rushwa.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Mwanamke azaa mapacha na kuwaita Barack Obama na Mitt Romney

Mwanamke mwenye miaka 20 Millicent Owuor jana amejifungua watoto mapacha na kuwapa majina Barack Obama na Mitt Romney.
Watoto hao walizaliwa katika hospitali ya Siaya kusini magharibi mwa Kenya.
Owuor aliwaambia waandishi wa habari kuwa aliamua kuwapa majina hayo wanae ili kuikumbuka siku ya uchaguzi huo wa Marekani.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA MTWARA-DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na viongozi wengine wakimsikiliza  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo miundombinu ya  bomba la gesi asilia toka Mtwara…
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali. 

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Hiki ndicho T.I anadhani kilikuwa chanzo cha ugomvi kati ya Rick Ross na Young Jeezy.

Rapper T.I ambae pia ni mshindi wa tuzo za Grammy amechangia mawazo yake kwa kile kilichotokea wiki hii ambapo Rick Ross the Big Boss alizinguana vibaya na Young Jeezy hadi kufikia hatua ya kusukumana walipokuwa back stage wakati wa kurekodi matukio ya BET Hip Hop Awards 2012.

katika interview moja T.I alitaja ‘majivuno na umimi’ kuwa mara nyingi ni chanzo cha celebs  kugombana, japo alionesha kuwa ni mtazamo wake na anavyodhani ila hakujua lolote kuhusu huo ugomvi kati ya Rick Ross na Young Jeezy.

“Hata sikujua kuhusu huo ugomvi.”alisema T.I kwenye hiyo interview na akaongeza kuwa “wanaume katika sehemu yoyote, huwa tuna umimi na majivuno kwa kiasi kikubwa sana. Sijui huu ugomvi personally lakini mara nyingi ugomvi ninaousikia hua unatokana na majivuno na umimi. Lakini siwezi kuzungumzia hili kwa kila ugomvi, na sijui mengi kuhusu huu ugomvi.” Alimasema hit maker wa Leave my Life.
 

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

DAIMOND SIKU YAKE YA KUZALIWA

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Chris Brown na Rihanna katika show ya Jay Z
Inasemekana ukaribu unaoendelea kuonekana kati ya R&B singer Chris Brown na Rihanna ukawa ni ukurasa mpya wa mapenzi yao ambayo bado hawajayaweka wazi kwa kauli zao.

Muda mchache uliopita Chris brown ametangaza rasmi kuachana na girl friend wake Karrueche Tran kwa madai kwamba hataki kuendelea kumuumiza kutokana na urafiki alionao na Rihanna. Uamuzi huo unakupa picha gani? Kama ni sacrifice kwanini hakuamua kustay away from Rihanna ili asimuumize girl friend wake huyo??? haya ndio maswali yanayowafanya watu wengi waamini kuwa Chris and Rihanna are back together.

"Nimeamua kuwa single, ili niweze ku focus katika kazi yangu. Nampenda sana Karruche lakini sipendi kuona akiumia kutokana na urafiki wangu na Rihanna", hayo ni maneno aliyoyasema Chris Brown wakati akitoa maelezo ya kwanini kachukua uamuzi huo. Aliongeza kwa kusema "ni bora niwe single ili wote tuwe happy katika maisha yetu".

Uamuzi huo wa Chris Brown umekuja mara baada ya yeye na Rihanna kuonekana wakiwa pamoja katika concert ya Jay Z iliyofanyika Brooklyn usiku wa juzi kwa saa za marekani.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Vifo vya watoto vimepungua duniani

Watoto
Takriban watoto milioni 6.9 walifariki kabla ya kufikisha miaka mitano mwaka jana ikilinganishwa na vifo milioni 12 vya watoto wachanga vilivyotokea mwaka 1990. Takriban watoto elfu kumi na tisa walifariki mwaka 2011.
Kwa mujibu wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa mataifa Unicef, sababu mojawapo ya kupungua kwa vifo ni nchi maskini kutajirika.
Lakini, sababu nyinginezo ni nchi zinazostawi kupata msaada unaostahili kufanya kampeini za kuhamasisha wanawake kuwanyonyesha watoto na kuwapa chanjo.
Nchi ambazo idadi ilipungua sana ni zile ambazo zilipata msaada mwingi kutoka nje.
"ukiangalia, nchi ambazo idadi ya vifo imepungua sana mfano Jamuhuri ya watu wa Lao, Timor na Liberia
ambazo ni nchi tatu za kwanza katika orodha ya nchi ambako idadi ya vifo ilipungua, nadhani kwa nchi hizi zote msaada unaotoka nje umechangia pakubwa jambo hilo,'' alisema mkurugenzi mkuu wa shirika la Unicef nchini Uingereza, David Bull.

Juhudi zinazolenga magonjwa ya kuambukizana kama Ukambi, zimepunguza vifo duniani kutoka vifo vya watoto laki tano mwaka 2000 hadi vifo laki moja mwaka 2011.
Mwaka jana nusu ya vifo vya watoto wachanga duniani vilitokea katika nchi tano pekee kulingana na Unicef. Hizi nchi ni pamoja na India, Nigeria, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Pakistan na China.
Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chad, Somalia, Mali, Cameroon na Burkina Faso idadi ya vifo vya watoto iliongezeka kwa vifo 10,000 au zaidi mnamo mwaka 2011 ikilinganishwa na mwaka 1990.
Karibu vifo hivyo vyote vilichangiwa na ugonjwa wa Malaria kwa watoto walio chini ya miaka mitano katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara mwaka jana kwa mujibu wa shirika hilo. Mizozo pia ilichangia huku ugonjwa wa kichomi na tatizo la kuharisha vile vile nayo yakichangia vifo hivyo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS