WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Vifo vya watoto vimepungua duniani

Watoto
Takriban watoto milioni 6.9 walifariki kabla ya kufikisha miaka mitano mwaka jana ikilinganishwa na vifo milioni 12 vya watoto wachanga vilivyotokea mwaka 1990. Takriban watoto elfu kumi na tisa walifariki mwaka 2011.
Kwa mujibu wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa mataifa Unicef, sababu mojawapo ya kupungua kwa vifo ni nchi maskini kutajirika.
Lakini, sababu nyinginezo ni nchi zinazostawi kupata msaada unaostahili kufanya kampeini za kuhamasisha wanawake kuwanyonyesha watoto na kuwapa chanjo.
Nchi ambazo idadi ilipungua sana ni zile ambazo zilipata msaada mwingi kutoka nje.
"ukiangalia, nchi ambazo idadi ya vifo imepungua sana mfano Jamuhuri ya watu wa Lao, Timor na Liberia
ambazo ni nchi tatu za kwanza katika orodha ya nchi ambako idadi ya vifo ilipungua, nadhani kwa nchi hizi zote msaada unaotoka nje umechangia pakubwa jambo hilo,'' alisema mkurugenzi mkuu wa shirika la Unicef nchini Uingereza, David Bull.

Juhudi zinazolenga magonjwa ya kuambukizana kama Ukambi, zimepunguza vifo duniani kutoka vifo vya watoto laki tano mwaka 2000 hadi vifo laki moja mwaka 2011.
Mwaka jana nusu ya vifo vya watoto wachanga duniani vilitokea katika nchi tano pekee kulingana na Unicef. Hizi nchi ni pamoja na India, Nigeria, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Pakistan na China.
Katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chad, Somalia, Mali, Cameroon na Burkina Faso idadi ya vifo vya watoto iliongezeka kwa vifo 10,000 au zaidi mnamo mwaka 2011 ikilinganishwa na mwaka 1990.
Karibu vifo hivyo vyote vilichangiwa na ugonjwa wa Malaria kwa watoto walio chini ya miaka mitano katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara mwaka jana kwa mujibu wa shirika hilo. Mizozo pia ilichangia huku ugonjwa wa kichomi na tatizo la kuharisha vile vile nayo yakichangia vifo hivyo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: