Wananchi wakitoroka mapigano
Uingereza imesitisha
kwa muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu
kuhusika kwa nchi hiyo katika mzozo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
Mawaziri walisema kwamba Uingereza sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21.
Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha
pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba, hata baada ya tashwishi kuwepo
kuhusu tetesi kwamba ilikuwa inawaunga mkono wanamgambo wa M23 wa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali ya Uingereza ilikuwa imesema kwamba
ingetoa kitita kingine cha pauni milioni 18 kwa ajili ya mahitaji ya
kibandamu ya dharura huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Makubaliano
Sasa fedha hizo, ambazo zilikuwa zitolewe mwezi
ujao, hazitatolewa tena kwa sababu serikali ya Rais Paul Kagame imekiuka
makubaliano.
Nyaraka ya Umoja wa Mataifa iliyofichuliwa inasema kwamba waziri wa ulinzi wa Rwanda ndiye anayewaamrisha waasi walioko huko.
Mapigano hayo yamepingwa na nchi za kimataifa,
huku Marekani na nchi kadhaa za Ulaya zikizuia msaada uliokuwa umepangwa
kwa ajili ya Rwanda.
Waziri Justine Greening wa Uingereza alisema:
“Nimeamua kutotoa fedha zilizokuwa zimekusidiwa kwa ajili ya kuisaidia
bajeti ya Rwanda. Ni wajibu wetu kujaribu kutafuta suluhu za kudumu kwa
mzozo wa eneo hili, na kufanya kazi pamoja na serikali za Rwanda na
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kuhakikisha suluhisho la amani
linapatikana mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo." |
0 maoni:
Post a Comment