Generali Mamdou Shahin (Kulia) akishauriana na maafisa wa kamati ya katiba kabla ya kupigiwa kura
Kamati inayoandika katiba nchini Misri imeidhinisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Hayo yaliafikiwa katika shughuli iliyochukua saa
kumi na sita, na kamati hiyo ilikubaliana kwa kauli moja kupitisha
vifungu viwili thelathini na nne.
Rasimu hiyo sasa sharti iidhinishwe na rais Morsi kabla ya kupigiwa kura ya maoni.
Wanasiasa waliberali pamoja na wakristu walisusia shughuli za kamati wakisema walihisi kutengwa.
Akizungumza kwa runinga awali Rais Mohamed Morsi
amesema kuwa atajiondolea mamlaka mapya aliyojikabidhi pindi tu watu
watakapokubaliana kuhusu katiba. |
0 maoni:
Post a Comment