WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

SAJUKI AONDOKA LEO KUELEKEA NCHINI INDIA KWA MATIBABU

Wednesday, May 9, 2012

BAAADA YA KUPATIKANA KWA KIASI FULANI,SAJUKI SASA KUONDOKA.!

Msanii wa filamu Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki ambaye anasumbuliwa na maradhi ya uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa anaondoka nchini leo kuelekea India kwa matibabu yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo na kukosa matibabu hapa nchini. Safari ya msanii huyo imekuja baada ya wadau wa filamu, wasanii na
watu mbalimbali kujitolea kwa nyakayi tofauti ili kuweza kufanikisha matibabu ya msanii huyo wa siku nyingi ambaye pia ni Director, Jumla ya Tsh. 16 milioni ziliweza kupatikana huku ikiwa bado inahitajika Tsh. 9 milioni ili kukamilisha kiwango kilichokusudiwa kukusanywa kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo, na pia ziliweza kupatikana tiketi tatu za ndege za kwenda na kurudi nchini India.Tunakutakia kila la kheri Sajuki na Mungu akubaliki shukrani nyingi kwa waliojitolea kumsaidia mwenzetu kupata nafasi ya kwenda kutibiwa.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: