WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

BASI LAUNGUA MOTO MJINI MOROGORO

BASI LA MURO LATEKETEA KWA MOTO LIKIWA LINATOKEA TABORA KUJA DAR!.


Basi lenye namba za usajiri T 820 BEY mali ya kampuni ya Muro Investment lililokuwa likitokea Tabora kuja jijini  Dar es salaam limeteketea kwa moto maeneo ya maseyu Mkoani Morogoro majira ya saa moja usiku wa tarehe 8 may. Basi hilo lililokuwa na abiria 65 lilipata hitilafu kwenye mfumo wake wa umeme uliosababisha shoti iliyoanzisha moto maeneo ya uvungu wa gari hilo, ambapo lilipofika eneo la
tukio wananchi waliokuwa chini waliweza kuliona na kupiga kelele ambapo dereva alisimamisha gari hilo, hakuna aliyejeruhiwa wala kufariki kwani abiria wote waliweza kushuka salama baada ya gari hilo kusimama lakini mizigo na mali zote ndani ya gari hilo ziliteketea kwa moto.


 
 Hao ni wakazi wa kijiiji kimoja nje kidogo ya mji wa morogoro wakiwa wanashangaa kuona maajabu hayo Dj Daffa alipata kuzngumza na mkazi mmoja jina limehifadhiwa na hii blog na akasema ukaguzi wa vyombo vya moto kabla ya kuondoka umekuwa ukadhalauliwa sana na nikama hivyo sasa mali za abiria zimetekeketea lawama kwa nani mmliki wa kampuni hiyo au serikari mkazi huyo akiongea kwa jazba sana huku kusisitiza wakaguzi wa vyombo vya moto wawe makini kuchunguza vyombo hivyo kabla ya kuondoka ili kuhakikisha usalama wa abiria na mali zao

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: