WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

malawi kubariki ushoga

RAIS wa Malawi, Joyce Banda, amesema kuwa nchi hiyo itabadili sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja, hivyo kuruhusu ndoa ya jinsi moja.
Banda alitoa kauli hiyo wakati akilihutubia taifa kwa mara ya kwanza jana tangu atawazwe kuwa Rais wa nchi hiyo.
Mageuzi hayo yataifanya Malawi kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kubariki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja tangu mwaka 1994.
Viongozi kadhaa wa nchi za Magharibi hivi karibuni walisema kuwa wataziondolea misaada nchi ambazo hazitambui haki za mashoga na wasagaji.
Kauli ya Rais Banda ambaye aliingia madarakani mwezi uliopita imekuja baada ya wanaume wawili wa Malawi kuhukumiwa kifungo cha miaka 14 jela mwaka 2010 baada ya kusema kuwa walikuwa wakifunga ndoa.
Baada ya kimbunga cha shutuma kutoka kwa mataifa makubwa, Mutharika aliwasamehe wanaume hao kwa sababu ya mazingira ya kibinadamu lakini alikaririwa akisema: “Wanaume hao walikiri kuwa wamefanya uhalifu dhidi ya utamaduni wetu, dini zetu na sheria zetu.”
Rais Banda alichukua madaraka mwezi uliopita baada ya mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, kufariki kwa shambulio la moyo.
Tangu atawazwe kuwa Rais wa nchi hiyo, Rais Banda amefanya mabadiliko ya sera kadhaa za mtangulizi wake, ikiwa ni pamoja na kushusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo ikiwa ni moja kati ya matakwa muhimu ya Shirika la Fedha Duniani (IMF).
Hata hivyo katika nchi nyingi za Kiafrika mapenzi ya jinsia moja hayaruhusiwi na ni kosa kisheria kujihusisha nayo.
Nchini Uganda, Mbunge mmoja aliwasilisha muswada ambao unataka watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wapewe adhabu ya kifo.
Hata hivyo baada ya mataifa makubwa kuingilia kati na kukosoa kauli hiyo na hata kutishia kusitisha misaada yake, baadaye Mbunge huyo alibadili muswada wake na kutaka wafungwe kifungo cha maisha jela.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: