WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

OMBI LA LULU MEI 28 KUSIKILIZWA MAHAKAMA YA DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema Mei 28 ni siku ambayo itasikiliza ombi la msanii wa filamu nchini Eizabeth Michael ‘Lulu’anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Lulu anaiomba mahakama hiyo kuiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuipeleka kesi hiyo katika mahakama ya watoto kwa sababu mshtakiwa huyo ana umri wa chini ya miaka 18.
Kwa mujibu wa hati ya kuitwa mahakamani iliyotolewa na mahakama hiyo kwa mawakili wa pande mbili jana, inaonyesha Jaji Dk. Fauz Twaibu ndiye atakayesikiliza ombi hilo Na. 46/2012 ambalo limewasilisha Mei 15, mwaka huu, mahakamani hapo na wakili kiongozi anayemtetea Lulu, Kenned Fungamtama, chini ya hati ya dharura iliyokithiri.
Lulu anadai kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando wiki iliyopita alikataa kutoa uamuzi juu ya ombi la mawakili wake wakitaka kesi hiyo ihamishiwe mahakama ya watoto, baada ya hakimu huyo kusema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutolea uamuzi ombi hilo na kuwashauri mawakili hao kuwasilisha ombi hilo Mahakama Kuu.
Mei 7, 2012 mawakili hao waliwasilisha ombi hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakidai kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17, hivyo bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Kesi ya msingi iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itatajwa tena Mei 21, mwaka huu.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: