WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Idadi ya waliofariki yaongezeka Yemen

Mwanajeshi aliyejeruihiwa katika shambulio mjini Sanaa

Takriban wanajeshi 90 wameuwawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika mji mkuu wa yemen sanaa.

Zaidi ya wengine mia tatu walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea katika karibu na ikulu ya rais wakati wanajeshi walipokuwa wakijiandaa kwa gwaride la kijeshi.

Ripoti zinaarifu kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga naye alikuwa amevalia magwanda ya jeshi.

Duru kutoka kwa kundi la kigaidi la Al-Qaeda zinasema kuwa kundi hilo ndilo lilihusika na shambulizi hilo.

Jeshi la Yemeni hivi sasa linaendesha harakati za kijeshi dhidi ya kundi hilo kusini mwa nchi. I Hili ndio shambulii kubwa ziaid kutokea mjini Sanaa tangu rais Abd-Rabbuh Mansour kuchukua mamlaka mwezi Februari.

Mwanajeshi mmoja alielezea alichoshuhudia akisema kuwa waliohusika lazima wachukuliwe hatua, wito ambo pia ulitolewa na maafisa kadhaa wa jeshi.Add caption

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: