WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Maandamano nchini Mali

Maandamano Mali

Maelfu ya watu waliopinga mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, wameandamana kupinga mwafaka ulioafikiwa na shirika la ECOWAS, kwamba kiongozi wa kiraia wa mpito aweze kusalia uongozini kwa mwaka mmoja.

Hata hivyo muda wa kuongoza aliopewa kiongozi huyo, Djouncounda Traore ulitarajiwa kukamilika Jumatatu.

Lakini viongozi wa nchini za Magharibi, waliafikia mkataba na kiongozi wa mapinduzi Kapteni Amadou Sanogo kwamba bwana Traore asalie mamlakani ili aweze kuongoza harakati za uchaguzi na kumaliza harakati za waasi wa Tuareg.

Mkataba huo pia ulijumuisha mpango wa kukubalia Sanogo atajwe kama kiongozi wa zamani alipwe mshahara wa rais na apewe nyumba ya kifahari.

Mapinduzi hayo pamoja na harakati za waasi kuteka Kaskazini mwa Mali, yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao.

Mashirika ya misaada wanasema wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Mali nchi ambayo pia inakumbwa na baa la njaa.

Mwandishi wa BBC mjini Bamako, Martin Vogl amesema kuwa wanajeshi waliwaruhusu baadhi ya waandamanji kuingia katika ikulu ya rais ingawa bwana Traore hakuwepo wakati huo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: