WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Tetemeko lapiga kaskazini mwa Utaliana

Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa eneo la kaskazini mwa Utaliana, na kuuwa watu kama 5, na kusababisha uharibifu.


Tetemeko hilo lilisikika sehemu kubwa ya kaskazini, lakini kitovu chake kilikuwa karibu na mji wa Modena.

Picha za televisheni kutoka eneo la tetemeko zimeonyesha nyumba zilizoporomoka, pamoja na minara ya makanisa ya kale.

Vifo vitatu vilivothibitishwa, vimetokea katika kiwanda kimoja kilichoporomoka kwenye tetemeko hilo, na kuna wasiwasi kuwa watu wengi zaidi pengine wamekwama chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Tetemeko lilikuwa namba 6 kwa kipimo cha Richter.

Imearifiwa kuwa mitetemeko midogo kadha imefuata.Add caption

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: