Februari tarehe kumi na nne ni siku ya wapendanao au
Valentine, lakini siku hii ikiadhimishwa kote duniani kwa raha, baadhi
ya waume nchini kenya hawaifurahi kwani wanapigwa na kunyanyaswa na wake
zao.
Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea
haki za wanaume nchini humo Nderitu Njogu, idadi ya wanaume wanaopigwa
na wake zao imeongezeka mno.
Bw Nderitu anasema utafiti wa chama chake
umeonyesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na
kuwasabibisha kuwadharau wanaume.
Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo
limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawake wengi sasa wana kipato
kikubwa kuliko waume zao.
Mwishoni mwa wiki Polisi walimtia mbaroni
mwanamke mmoja mjini Nyeri huko mkoa wa kati, baada ya kumshambulia
mumewe na kumjeruhi vibaya kwa panga.
Mwanamume huyo bado anapokea matibabu hospitalini baada ya kukatwa katwa usoni. uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.
Bw Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume 460,000
walinyanyaswa na wake zao mwaka jana. Anasema utafiti wa shirika lake
unaonyesha kesi nyingi za waume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika
mkoa wa kati.
"Siku hii ya Valentine na washauri wanaume
wasikubali kudhalalishwa na wake zao, kwa kufanya matumizi makubwa
kuliko na wanayoweza kumudu" alisema Bw Nderitu
0 maoni:
Post a Comment