WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Uzembe wa UN 'unachochea maafa Syria'

Mkuu wa tume ya kutetea haki za binadamu ya umoja wa mataifa Navi Pillay amesema kutokuwepo na msimamo imara kuhusu Syria katika baraza la usalama la umoja huo, kumechangia maafa zaidi ya raia.
Bi Pillay ameorodhesha aina mbali mbali za ukiukwaji wa haki za binadamu na akasisitiza kuwa amefadhaishwa sana na mashambulio ya raia katika mji wa homs.
Akizungumza mjini New York alitoa ushaidi kuonyesha kuwa majeshi ya Syria yanatekeleza uhalifu dhidi ya binadamu.
"Imekuwa vigumu sasa kwa ofisi yangu kuchukua takwimu ya vifo vilivyo tokea katika kipindi cha miezi miwili. Lakini tuna uhakika kuwa idadi ya waliokufa na waliojeruhiwa inaongezeka kila siku" amesema Bi Pillay
Kamishna huyo, alielezea bayana kuwa amechukizwa na mabalozi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambao wameshindwa kutoa kauli moja kuhusu Syria.
Amesema kuwa hali hii, imechochea utawala nchini humo kuzidisha mashambulio dhidi ya upinzani.
Matamshi makali ya Bi Pillay yalilenga kushinikiza utawala wa Rais Assad, Urusi na China- ambao walipiga kura ya turufu kupinga mswada huo dhidi ya Syria kwenye baraza la uslama- kubadilisha msimamo.
Lakini hakuna dalili zozote kuwa matamshi yake yatabadilisha mambo.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, ambaye alizuru Syria wiki iliopita, alisisitza kuwa suluhu ya mzozo huo itapatikana bila shinikizo kutoka nchi za kigeni.
"Tuna jukumu la kuwasaidia watu wa Syria. Ni kwa sababu hii tunahitaji kupanua majadiliano kati ya raia wa Syria ilikupata suluhu au uamuzi ambao utazingatia matakwa ya raia wote nchini humo bila kuingiliwa na wahusika wengine kutoka nje" alisema Bw Lavrov.
Baraza la uslama linajadili ripoti ya kamishna Navi Pillay, lakini awali balozi wa Syria katika Umoja wa mataifa, Bashar Ja'afari alijaribu kuvunja mkutano huo.
Balozi huyo alipata kuungwa mkono na wenzake kutoka Iran na Korea Kaskazini, lakini mwenyekiti wa baraza hilo alipinga kauli zao.
Bado kuna migawanyiko kwenye baraza hilo kuhusu suala la Syria na awali wanachama walikuwa na tashwishi kuhusu pendekezo la kuudwa kwa kikosi cha kulinda amani kitakacho jumuisha umoja wa mataifa na jumuiya ya nchi za kiarabu nchini Syria.


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: