11 Februari, 2012 - Saa 15:14 GMT
Rais mstaafu wa Ghana, John
Kufuor, ameiambia BBC kwamba ukame katika kanda ya Sahel ya Afrika
unaathiri watu kama milioni 12 katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Alisema ulimwengu haukujifunza
kutoka yale yaliyojiri Somalia, na unasubiri hadi watu wafe kwa njaa
kabla ya kutoa msaada wa kutosha.
Alieleza kuwa ukame unazusha mapambano nchini Ghana, baina ya wafugaji na wakulima:
"Tuna tatizo kubwa linaloendelea la wafugaji wanaohama kutafuta malisho.
Kila ukame ukikausha malisho katika Sahel, wafugaji wanaelekea kusini kwenye misitu, pamoja na Ghana.
Na siku hizi, kila ukifungua gazeti na kuskiliza
redio, kila siku unasikia mapambano baina ya wafugaji wa kabila la
Fulhani na wakulima."







0 maoni:
Post a Comment