18 Januari, 2012 - Saa 16:16 GMT
BBC imeona ushahidi wa mtu mmoja
kuteswa na kuuliwa akiwa kizuizini, baada ya mapigano baina ya
wapiganaji wapinzani nchini Libya mwishoni mwa juma.
Watu kutoka familia ya Izzedine al-Ghool wamesema alishutumiwa kwa kuunga mkono uongozi wa marehemu Kanali Muammar Gaddafi.
Waliokuwa makamanda waasi walisema
wameanzisha harakati mpya za kuwanyang'anya silaha waliomtii Gaddafi
waliopo maeneo ya Gharyan, kilomita 80 kusini mwa Tripoli.
Takriban watu tisa waliuawa katika mapigano yaliyotokea wiki iliyopita, maafisa walisema.
Waziri mkuu wa serikali ya mpito Abdurrahim
al-Keib na waziri wa ulinzi Osama al-Juweili walitembelea eneo hilo
katika jitihada za kusimamisha mapigano.
'Mshtuko wa umeme'
Mapigano hayo yanasemekana kuibuka baada ya
wapiganaji wa Gharyan walipowakamata watu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano
na uongozi wa marehemu Gaddafi kwenye mji wa Assabia, takriban kilomita
16 kusini- magharibi mwa nchi hiyo.
Imeripotiwa wapiganaji wa Assabia walikataa
kuwakabidhi washukiwa, na kuchochea mapigano ambapo roketi na bunduki
nzito za rashasha zilirushwa.
Mwandishi wa BBC Gabriel Gatehouse, mjini
Tripoli, aliripoti familia ya Bw Ghool ilisema alikuwa kamanda wa kikosi
maalum cha wapiganaji kwenye eneo lake la asili Assabia, na alitiwa
kizuizini siku ya Ijumaa baada ya mapigano kuanza.
Lakini wamekanusha kuwa bado alikuwa na utii kwa uongozi uliopita.
Kwa sasa mwili wake umewekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye mji mkuu.
BBC imeona alama kwenye miguu na makalio yake inayoashiria kuwa aliteswa sana.
Mwandishi wetu alisema hili ni suala nyeti kwa uongozi wa mpito.
Ofisa wa jeshi katika chumba hicho cha kuhifadhi
maiti aliikatalia BBC ruhusa ya kumhoji daktari aliyefanya uchunguzi wa
maiti hiyo.
Lakini muuguzi aliyekuwepo wakati mwili huo
ulipofanyiwa uchunguzi alisema Bw Ghool aliadhibiwa kwa mshtuko wa umeme
na kupigwa kupita kiasi.
Siku ya Jumapili, kamanda wa jeshi la Gharyan alisema watu wake waliteka idadi kadhaa ya wafungwa, ambapo mpaka sasa wameachiwa
0 maoni:
Post a Comment