15 Februari, 2012 - Saa 21:12 GMT
Takriban wafungwa 300 wameuwawa katika moto ulioteketeza jela moja nchini Honduras kwa mujibu wa maafisa wa serikali.
Wengi wao waliteketea au kukosa hewa katika seli zao za jela ya Comayagua, kaskazini mwa mji mkuu Tegucigalpa.
Maafisa wa serikali wanasema
imethibitishwa takriban 300 wamekufa lakini wengine 56 kati ya wafungwa
853 katika gereza hilo hawajapatikana na inadhaniwa wameteketezwa.
Jamaa wa wafungwa hao walipambana na polisi pale
walipojaribu kuvamia jela hiyo wakitafuta maelezo zaidi ya majaaliwa ya
watu wao.
Polisi walipaswa kufyatua risasi hewani na
kutumia gesi ya kutoa machozi. Uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha
moto huo kama ulisababishwa na hilitalfu katika nyaya za umeme ama
zilichochewa na ghasia za wafungwa.
Rais Lobo wa Honduras ameahidi uchunguzi kamili ulio wazi na kusema hillo ni janga lisilokubalika.
Alisema wakuu wa magereza wa kitaifa na wa eneo la moto huo watasimamishwa kazi wakati uchunguzi ukiendelea.
Wafungwa wengine wanatibiwa majeraha makali ya moto kwenye hospitali mjini Tegucigalpa
0 maoni:
Post a Comment