Mmoja wa waliojeruhiwa wakitafuta ajira huko Tunisia
Zaidi ya watu mia
mbili walijeruhiwa huko Tunisia Jumatano katika siku ya pili ya
maandamano jijini Siliana kilomita mia moja Ishirini kutoka katika jiji
kuu la Tunis.
Waandamanaji hao walikuwa wakimtaka gavana wa
eneo hilo kujiuzulu, kutaka msaada wa kiuchumi na vile vile kushinikiza
watu kumi na wanne waliokamatwa katika ghasia za Aprili kuachiliwa.
Maafisa wa usalama walitumia gesi ya
kutoa machozi na risasi za mipira kuwatwanya watu waliokuwa wanataka
ajira. Pia kulikuwa na ripoti za watu kutibiwa baada ya kupata majeraha
ya risasi.
Vyama vya wafanyakazi vimeitisha maandamano zaidi baadaye leo.
Tunisia ndiyo ilikuwa kitovu cha mapinduzi ya
kiraia katika nchi za Kiarabu ambapo wananchi walimng'oa mamlakani rais
wao wa muda mrefu Januari mwaka 2011. |
0 maoni:
Post a Comment