WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Wachimba migodi 30 wapigwa risasi

Polisi wawafyatulia risasi wachimba mgodi
Zaidi ya watu 30 wauwawa katika makabiliano kati ya polisi na wachimba migodi wanaogoma Afrika kusini.
Waziri wa Polisi wa Afrika kusini amesema maafa hayo yalitokea siku ya Alhamisi katika mgodi wa Marikana.
Polisi walifyatua risasi baada ya kushindwa kuwatawanya wagomaji hao waliokuwa wamejihami kwa marungu na mapanga.
Mgodi huo wa dhahabu nyeupe unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin imekuwa ni sehemu ya mapigano makali kuhusu mzozo wa malipo uliotokana na uhasama kati ya vyama viwili vya wafanyakazi.
Kisa hicho cha polisi ni moja wapo wa operesheni mbaya zaidi ya polisi tangu kumalizika kwa enzi za ubaguzi wa rangi.
Awali machafuko hayo yalioanza wiki iliyopita yalikuwa yamesababisha vifo vya watu 10 na polisi wawili.
Siku ya Ijumaa waziri wa Polisi ,Nathi Mthethwa akizungumza na kituo kimoja cha Radio alithibitisha kuwa watu wengi walijeruhiwa na wengine kuuwawa.
Chama kikuu cha wachimba migodi, National Union of Mineworkers ,kinasema idadi ya waliofariki ni 36.
Polisi walikuwa wamepelekwa kwenda kuwatawanya wachimba migodi wapatao 3,000 ambao walikuwa wamekusanyika eneo la mlima mkabala na mgodi wa Marikana, ambao uko kilomita 100 kaskazini mangharibi mwa Johannesburg.
Wafanyakzi hao walikuwa wanataka nyongeza ya mshahara ya dola $1,000 kila mwezi.
Mazingira yaliofanya polisi waanze kufyatua risasi bado haijajulikana , lakini taarifa kutoka kwa walioshuhudia zinasema mauji hayo yalitokea wakati kundi la waandamani walipojaribu kuwavamia polisi.
Hapo ndipo polisi waliokuwa wamejihami kwa bunduki na bastola wakaanza kufyatua risasi.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: