WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Vibonzo vyachapishwa A Kusini

Hatua ya kundi moja la Kiislamu nchini Afrika Kusini kuzuia uchapishaji wa vibonzo vya mtume Muhammed imeshindikana.
Kibonzo hicho kilichochorwa na Jonathan Shapiro, ajulikanaye kama Zapiro, inamwonyesha mtume akiwa kwenye kiti cha madaktari wenye maradhi ya akili akilalamika kuwa wafuasi wake hawapendi maskhara au utani.
Ameichora kufuatia mtandao wa kijamii wa Facebook kuwakaribisha watu wachore taswira za Mtume Muhammed, iliyosababisha Pakistan kupiga marufuku tovuti kwa kuwa "kinyume na uislamu."

'Tishio la Kombe la Dunia'

Baraza la wanaotoa elimu ya dini ya Kiislamu la Afrika Kusini, lijulikanalo kama Jamiatul Ulama, limesema kibonzo hicho kilichochapishwa kwenye gazeti la Africa Mail na Guardian ni jambo la kuchukiza.
Limesema katika nyaraka ilizowasilisha mahakamani kuwa muda ambao kibonzo hicho kimetolewa huenda ikaleta hatari wakati wa Kombe la Dunia.
Lakini mahakama kuu imetoa uamuzi kuwa kibonzo hicho tayari kilishachapishwa hadharani katika tovuti ya Mail na Guardian.
Uislamu hauruhusu michoro ya Mtume au Allah na vibonzo vya Mtume Muhammed vilivyochapishwa katika gazeti la Denmark mwaka 2006 vilisababisha maandamano duniani kote kupinga hatua hiyo.
Kwa wakati huo, Jamiatul Ulama ilifanikiwa kuzuia vibonzo hivyo vya Denmark kuchapishwa tena katika gazeti la Afrika Kusini la Sunday Times.

'Sema kweli'

Bw Shapiro alitetea kitendo chake cha kuchora vibonzo hivyo katika mahojiano ya BBC.
Amesema, "Kibonzo si kibaya hivyo ina viashiria vya huruma."
"Ni kama namna ya kuwaambia watu waseme, 'Haya, muishi kwenye uhalisia, hii ni karne ya 21."
Amesema wakati wa maandamano ya mwaka 2006, aliamua kutokuchora vibonzo vyovyote vya Mtume.
"Sitofanya hivyo kwasababu tu nimeamua, sijajaribu kuchochea lolote kwa makusudi- wakati kama huu nimejiunga na kampeni ya kimataifa."
Mhariri wa Mail na Guardian Nic Dawes amesema, "Kama tungetakiwa kuzuia kila kibonzo cha maudhi kinachochorwa na Zapiro, tusingekuwa na vibonzo vyovyote vya Zapiro kwenye gazeti."


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: