WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Mauwaji mjini Maiduguri ni magenge

Afisa wa ngazi ya juu wa forodha nchini Nigeria ameuawa kaskazini mashariki mwa nchi hio na watu waliokua na silaha.
Wakaazi wa Maiduguri wakimbia
Wakaazi wa Maiduguri wakimbia
Wakuu wa huko wanalishuku kundi la Boko haramu ambalo pia limetuhumiwa kwa mauwaji ya Wakristu wanne na pia kiongozi wa dini ya Waislamu Jumatatu iliyopita.
Watu sita waliokua na silaha walimvamia afisa huyo wa forodha Adamu Ahmadu nyumbani kwake usiku wa kuamkia jumatano huko Potiskum katika Jimbo la Yobena kumuua na vilevile kuwajeruhi wengine kwa mujibu wa polisi.
Wakuu wanalishuku kundi la Boko Haramu ambalo limekua likiwalenga maofisa wakuu kuhusika.
Katika Jimbo lililo jirani la Borno ambako kuna ngome ya kundi hilo, polisi ilidai kua kundi hilo liliua wakristu wanne siku chache baada ya msemaji wa Boko Haramu kuonya kua watawateketeza Wakristu kutoka baadhi ya maeneo ya nchi.
Wapighanaji hao wenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda pia walituhumiwa kwa kifo cha kiongozi wa Kiislamu katika mji mkuu wa Borno Maiduguri mnamo siku ya jumatano.
Wakati huo huo shirika la kimataifa linalochunguza haki za binadamu linasema kua takriban wanafuinzi elfu tano wamo njiani kurudi makwao baada ya shule 12 kuchomwa moto huko Maiduguri.
Shirika hilo linalilaumu kundi la Boko haramu , ingawa Kikosi maalum cha jeshi la Nigeria, kilichodai kuwaua watu watatu na wengine waliokamatwa wakijaribu kuchoma moto shule huenda ni magenge ya wahalifu wa huko ndio waliohusika na matukio ya hivi sasa.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: