WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Sudan: Marais wakutana Addis Ababa


Marais wa Sudan Kusini na Sudan wanakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia katika juhudi za kutafuta suluhu kwa tofauti zilizoibuka kati ya majirani hao wawili kuhusu mafuta.

Tangu kujitenga kwake kutoka kwa Sudan, Sudan Kusini imekuwa ikisafirisha mafuta yake kwa mauzo ya nje ya nchi kupitia mabomba ya Sudan.

Hata hivyo makubaliano ya kiwango cha malipo ya gharama ya uchukuzi hayakuafikiwa.

Sudan imelazimika kuchukua bila ruhusa mafuta hayo au kama inavyodai Sudan Kusini kuyaiba.

Kujibu vitendo hivyo Sudan Kusini ilitangaza kusitisha uzalishaji wa mafuta na kutengeneza bomba jipya la kusafirisha mafuta yake kupitia bandari ya Lamu nchini Kenya hatua ambayo huenda ikaathiri uchumi wa mataifa hayo mawili.

Ni kwa maana hii viongozi wa mataifa hayo mawili wanakutana.

Marais wa Kenya na Ethiopia wanaohudhuria mkutano huu watajaribu kuwapatanisha mahasimu hawa wa jadi. Inahofiwa kama hilo halitafanyika kutazuka mzozo mkubwa kati ya majirani hawa.  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: