Marehemu John Stephano Maganga, wakati wa uhai wake.
Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu
yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale
wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya,
ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza
gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, ameelezea
mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake
jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.
Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji
John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza
jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na
kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha anaendelea na kusema siku ya pili yake John alimpigia simu na
kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii vizuri, kuona hivyo, baba yake
mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta amelala kwenye kochi anatoka
jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?, John akamjibu, tumbo linamuuma
sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake mzazi nimwambie tumpeleke Hospital
Mwananyamala.
Tulipofika pale hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari
wakaamua wampige X Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu
makali sana tumboni mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari,
wakasema ana matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji
wa haraka.
Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi
na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za
kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili
kwa matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa
kwenye gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura
(emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye
tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi
kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo
walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu ambayo inaonekana
kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo vinaonesha ina
matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo maana
anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.
Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu
wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na
kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi
turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi nilifika Muhimbili na
kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku wa jana yake.
Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha kinachoendelea.
Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu yule daktari
ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani anamshughulikia hivyo
alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza punguza makali ya sumu
iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip ya maji lakini
inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.
Muda mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena,
amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake. Mazishi
yamepangwa kufanyika makaburi ya kinondoni kesho. Alisema baba mdogo
wa muigizaji Stephano. |
0 maoni:
Post a Comment