WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Hiki ndicho T.I anadhani kilikuwa chanzo cha ugomvi kati ya Rick Ross na Young Jeezy.

Rapper T.I ambae pia ni mshindi wa tuzo za Grammy amechangia mawazo yake kwa kile kilichotokea wiki hii ambapo Rick Ross the Big Boss alizinguana vibaya na Young Jeezy hadi kufikia hatua ya kusukumana walipokuwa back stage wakati wa kurekodi matukio ya BET Hip Hop Awards 2012.

katika interview moja T.I alitaja ‘majivuno na umimi’ kuwa mara nyingi ni chanzo cha celebs  kugombana, japo alionesha kuwa ni mtazamo wake na anavyodhani ila hakujua lolote kuhusu huo ugomvi kati ya Rick Ross na Young Jeezy.

“Hata sikujua kuhusu huo ugomvi.”alisema T.I kwenye hiyo interview na akaongeza kuwa “wanaume katika sehemu yoyote, huwa tuna umimi na majivuno kwa kiasi kikubwa sana. Sijui huu ugomvi personally lakini mara nyingi ugomvi ninaousikia hua unatokana na majivuno na umimi. Lakini siwezi kuzungumzia hili kwa kila ugomvi, na sijui mengi kuhusu huu ugomvi.” Alimasema hit maker wa Leave my Life.
 

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: