Mahakama nchini
Misri imemhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani waziri mkuu wa zamani
wa nchi hiyo Ahmed Nazif.
Nazif amehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ufisadi.Mwaka jana Ahmed Nazif alifutwa kazi kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kushtakiwa kwa kosa la kupata faida haramu kutokana na biashara alizofanya kinyume na sheria. Nazif alikuwa mmoja wa maafisa wakuu katika serikali ya rais wa zamani Hosni Mubarak. Alikamatwa miezi kadhaa baada ya kuacha kazi mwezi Januari mwaka 2011, muda mfupi kabla ya rais Mubarak kuachia ngazi. Maafisa kadhaa wa uliokuwa utawala wa Mubarak wamefikishwa mahakamani kwa aidha kosa la njama ya kuwaua waandamanaji au makosa kuhusiana na ufisadi. Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwezi Juni baada ya kuhusishwa na mauaji ya waandamanaji. |
Waziri mkuu wa zamani Misri afungwa jela
Posted by
RAMADHANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment