Rais wa Afrika Kusini Jacob
Zuma ametangaza kipindi cha maombolezo nchini humo kufuatia mauaji ya
wachimba madini thelathini na wanne yaliyofanywa na polisi,
Bwana Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya
kisheria ichunguze mauaji hayo katika mgodi wa madini meupe yaani
PLATINUM eneo la Marikana.wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi. Wakati huohuo wachimba madini wameamriwa kurejea kazini siku ya Jumatatu la sivyo watafukuzwa kazi. Lakini wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na kuwadhalilisha wenzao waliouawa. Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea kushinikiza malipo bora zaidi ya kazi. Hata hivyo chama cha wafanyakazi wa migodi cha NUM ambacho kina uhusiano wa karibu na chama tawala cha ANC - kinasema wanachama wake wamekubali kurejea kazini. Mmoja wa wachimba madini hao Vuyisile Mchiza, amesema atarejea kazini iwapo idadi kubwa ya wenzake watakubaliana kusitisha mgomo. ''Iwapo idadi kubwa watarejea kazini kesho, basi na mimi nitakwenda''. Anasema. ''Iwapo wengi hawatakwenda kazini, nami pia sitakwenda, kwasababu sitaweza kufanya kazi wakati wengine wakiwa bado wanaomboleza''. Ameongeza. |
Zuma atangaza maombolezo Afrika Kusini
Posted by
RAMADHANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment