WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Wasichana watakiwa kuvaa makoti India

Maandamano dhidi ya ubakaji India
Chama cha upinzani cha India, BJP, kimeiomba serikali ya mji wa Pondicherry, kusini mwa nchi, kuwapatia watoto wa shule makoti wavae ili wasinyanyaswe kijinsia. Katibu wa chama alitoa taarifa kusema kuwa unyanyasaji ni tatizo hasa katika shule za serikali, na kwamba wasichana wote wapewe makoti na piya wapate fursa ya kueleza malalamiko yao bila ya kujitambulisha.
Visa vya ubakaji vimezidi kuripotiwa nchini India na kupelekea sheria mpya kupitishwa.
Lakini baadhi ya viongozi wamelaumiwa kwa kutazama maisha ya wanawake tu, badala ya kubadilisha tabia za wanaume.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: