WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Urusi yazinga azimio kuhusu Qusair

Mwanaharakati wa Qusair akitembea katika mji huo unaoshambuliwa na jeshi la serikali ya Rais Assad
Wanabalozi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanasema kuwa Urusi imezinga mswada wa azimio la kueleza wasiwasi kuhusu hali, hasa ya raia, kwenye mji wa Syria wa Qusair ambao umezingirwa.

Mashambulio ya serikali dhidi ya mji huo unaodhibitiwa na wapiganaji yameendelea kwa zaidi ya majuma mawili na wakaazi wamenasa bila ya chakula, maji wala madawa.
Lakini wanabalozi wanasema Urusi haitaunga mkono mswada huo wa azimio kwa sababu Umoja wa Mataifa haukushughulika wakati mji huo ulipotekwa na wapiganaji.
Hapo jana Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, yalitoa maombi kuwa wasaidizi waruhusiwe kuingia Qusair.
Msemaji wa ICRC, Dibeh Fakhir, aliiambia BBC taarifa wanazopata kuhusu hali katika mji huo:
" Ripoti tunazopata zinasema kuna upungufu mkubwa wa maji, chakula na madawa.
Piya zinaeleza kuwa mamia ya raia wamejeruhiwa na hawawezi kupata matibabu.
Maelfu tayari wameshakimbia Qusair na maelfu wanasaidiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Syria, likisaidiwa na ICRC na mashirika mengine.
Hata hivo inaripotiwa maelfu bado wako ndani ya mji - kati yao ni mamia waliojeruhiwa vibaya lakini haiwezekani kuwatibu"
Alisema kuweza kusaidia inavyotakiwa, ICRC inahitaji kuwepo Qusair bila ya kuingiliwa kati na serikali.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: