WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya

Magwanda ya mabomu ya kujilipua
Polisi nchini Kenya wamenasa magwanda yenye mabomu ya kujilipua pamoja na zana zengine ambazo zilikuwa zitumike kwa mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi.
Washukiwa wawili wamekamatwa katika msako huo uliofanywa asubihi ya leo katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.
Msemaji wa polisi nchini Kenya Eric Kiraithe anasema kuwa maguruneti kumi na mbili pamoja na bunduki aina ya AK 47 pia zilinaswa wakati wa msako uliofanywa na polisi mtaani humo.
"tunaamini kuwa silaha hizi zilinuiwa kutumika kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi'' alisema bwana Kiraithe.
Msako huo uliofanywa na polisi Ijumaa uliongozwa na polisi wa kupambana na ugaidi baada ya polisi kupata habari kutoka kwa raia.
Na baada ya masaa kadhaa ya kuwahoji washukiwa, magwanda manne ya mabomu ya kujitoa mhanga , mabomu mawili na silaha zingine zilipatikana ndani ya nyumba ya mshukiwa mmoja.
Polisi wanaamini kuwa mabomu hayo yalikuwa na vilipuzi vyenye uzito wa kilo arobaini na yangetumika kushambulia baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi na miji mingine mikubwa.
Bwana Kiraithe amelaumu kundi la Al Shabab. Amesema kuwa washukiwa wengine 8 wako mbioni baada ya washukiwa Abdul majid Mohammed raia mkenya na Suleiman Abdi Aden msomali, kukamatwa na polisi wa Kenya.
Wangali wanahojiwa na polisi na watafikishwa mahakamani baadaye wiki ijayo.
Silaha hizo zinasemekana kufanana na zile zilizotumika katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Uganda dhidi ya watu waliokuwa wanatazama fainali ya kombe la dunia mwaka 2010, ambapo watu 76 waliuawa
Kundi la Al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi nchini Uganda, wakisema kuwa wanapinga nchi hiyo kujihusisha na harakati dhidi ya kundi hilo nchini Somalia.
Kenya imeshambuliwa karibuni na kundi la al-Shabab baada ya kupeleka vikosi vyake Somalia.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: