WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Clinton azungumza na viongozi wa Kenya

4 Agosti, 2012 - Saa 12:46 GMT

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, amekutana na viongozi wa Kenya katika sehemu ya mwisho ya safari yake ya Afrika.

Hillary Clinton alifanya mazungumzo na Rais Kibaki na Waziri MKuu Raila Odinga.
Bi Clinton alisema mazungumzo yake yalihusu maswala kadha pamoja na uchaguzi wa mwaka ujao nchini Kenya, na hali katika nchi ya jirani, yaani Somalia, ambako wanajeshi wa Kenya wanapigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab.
Bibi Clinton anaarifiwa kuiambia Kenya kuwa Marekani iko tayari kuisaidia Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, na Marekani inataraji uchaguzi huo utafanywa kwa salama.
Bibi Clinton piya alitarajiwa kukutana na wawakilishi wa serikali ya mpito ya Somalia walioko Nairobi.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: