WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

BOB JUNIOR ATUPIWA ZIGO LA LAWAMA

Mashabiki wa nyota wa muziki wa Kizazi kipya Bongo Junior wamemtupia zigo la lawama bosi huyo wa lebo ya sharobaro kwa kuwalaghai na kushindwa kutimiza ahadi kumwonyesha mke wake mtarajiwa wakati wa shoo yake aliyofanya ndani ya ukumbi wa Club Bilicannas jijini Dar. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Teentz.com mashabiki hao wlaiojitambulisha kuwa ni wakazi wa Gongo la Mboto walisema kuwa wameshindwa kumuelewa Bob Junior kwa kushindwa kuwaonyesha shemeji yao na kisha kukaa kimya bila kusema lolote tangu kufanyika kwa shoo hiyo jumapili iliyopita.
"Binafsi sikupendezwa na hali hile kwani licha ya kuja kuburudika, nia yangu kubwa ilikuwa ni kumuona mkewa wa Bob Junior msanii ambaye kwangu mimi ninamkubari kuliko wengine wote waliopo kwenye game" alisema mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kwa jina la Mudi.
Akiendelea zaidi Mudi alilalamika kuwa inavyoonekana ni kama Bob aliamua kuwadanganya watu juu ya jambo hilo ili apate watu wengi kwenye Shoo yake.
Hata hivyo mpaka habari hii inakwenda hewani jubudi za Teentz .com kumsaka Bob ili azungumze kuhusiana na tuhuma hizi hazijafanikiwa

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: