WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Vikosi vya EU vyashambulia maharamia

Baadhi ya meli zilizotekwa na maharamia pwani ya Somalia
Vikosi vya wanamaji wa EU, vimefanya shambulio lao la kwanza dhidi ya maharamia wa kisomali katika nchi kavu na kusema wameharibu baadhi ya maboti za maharamia hao.
Vikosi hivyo vilisafirishwa kwa helikopta hadi katika kitovu cha maharamia hao katika bandari ya Haradhere.
Vikosi vinavyopambana na maharamia havijakuwa vikipambana na maharamia katika maeneo ya nchi kavu , wakihofia kukamatwa kwa wafanyakazi wa meli hizo.
Maharamia nchini Somalia wamekamata meli kadhaa katika bahari hindi na wao hutaka kutolewa kwa kikombozi kwanza kabla ya kuachiliwa kwa meli hizo.
Kwa sasa wanadhaniwa kuteka takriban meli 17 na wafanyakazi 300 wa meli hizo.
Kisa cha hivi karibuni cha kukamatwa kwa meli kimehusisha meli ya ugiriki ya mafuta 'Smyrni' ambayo ilitekwa katika bahari ya Arabia wiki jana.
Meli hiyo ambayo ina bendera ya Liberia, imebeba tani 135,000 za mafuta ikielekea nchini Somalia.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya usalama, Frank Gardner anasema kuwa shambulio hilo ni hatua muhimu katika vita dhidi ya maharamia.
Hii ni mara ya kwanza, tangu EU kushika doria katika pwani ya Somalia tangu Disemba mwaka 2008.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: