WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Mlipuko mkubwa watokea jijini Nairobi

Mlipuko watokea mtaa wa Moi Nairobi na kujeruhi watu kadhaa
Mlipuko umetokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku majengo majengo yakiwa yanawaka moto.
Mlipuko huo umetokea ktika jengo lenye maduka madogo madogo mengi. Mwandishi wa BBC anasema mlipuko huo umesababisha bidhaa mbali mbali kama viatu, nguo na vioo vilivyovunjika kusambaa sehemu yote ya eneo hilo.
Mwandishi wetu Ramadhani Daffa anasema Polisi wamelizungushia eneo hilo uzio wa utepe kwa ajili ya usalama. Ni mapema kutaja idadi ya majeruhi lakini vyombo vingine vya habari vinasema zaidi ya watu 28 wamejeruhiwa na mlipuko huo
Picha za Televisheni nchini humo zimeonyesha watu wakikimbia mbali na majengo yaliyo karibu katikati ya mji wa Nairobi.
Kamishna wa Polisi nchini Kenya Mathew Iteere, anasema huenda "hitilafu ya umeme" ndio chanzo cha mlipuko huo, kwa mujibu wa Televisheni ya NTV. Hata hivyo mlipuko huo unaiweka Nairobi katika hali ya wasiwasi.
Kumekuwa na milipuko kadhaa hivi karibuni ndani na nje ya mji huo mkuu huku baadhi ikihusishwa na kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab.

Polisi waweka kizuizi eneo la mlipuko Nairobi
Timu ya waokoaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu imetumwa katika eneo la tukio kwenye mtaa huo wa Moi. Mtaa huo ni barabara kuu ambayo wakati wa mchana huwa na watu wengi, Shirika la habari la AP linasema.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia kulikuwa na mlipuko mkubwa na huku vipande vipande vya vioo na vitu vingine vikiwarukia na kujeruhi watu waliokuwa karibu, Gazeti la Nation linaripoti.
Gazeti hilo linaongeza kuwa mlipuko huo umetikisa majengo yaliyo karibu na harakati za kuwahamisha watu zimeanza.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: