Mapigano yamezuka katika mji wa
Port Said nchini Misri na kijana mmoja amekufa, baada ya timu ya mji huo
kupigwa marufuku kwa miaka miwili kufuatia ghasia za mwezi Februari,
zilizouwa watu zaidi ya 70.
Inaarifiwa kuwa polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na kufyatua risasi hewani.
Adhabu hiyo ya klabu ya al-Masry kukatazwa kucheza kwa miaka miwili, imetokana na ghasia zilizozuka katika uwanja wa timu hiyo ilipopambana na al-Ahly ya mjini Cairo.
Wamisri wengi wanawalaumu askari wa uslama kwa kutozimua ghasia za mwezi Februari.
0 maoni:
Post a Comment