Majususi wa Ufaransa
wamemkamata mtu wanayeamini kuwa mshukiwa wa mauaji ya watu wanne
wakiwemo, watoto watatu wa kiyahudi na mwalimu wao.
Mshukiwa huyo pia anaaminika kuwaua wanajeshi watatu.Kwa mujibu wa kituo cha televisheni BFM, wametoa tangazo kumtaja mshukiwa huyo wakisema kuwa amezuiliwa ndani ya jengo lenye nyumba nyingi ambalo walilizingira tangu ashubuhi ya leo. Muhammed Merah, ana umri wa miaka ishirini na nne, raia wa Algeria Wakati mmoja mshukiwa huyo alitupa nje bunduki moja ingawa waziri wa mambo ya ndani Claude Gueant, anasema mtu huyo angali amejihami vikali. Bwana Merah alizungumza na polisi wanaomshawishi mtu huyo kujisalimisha lakini baadaye akaodnoka kwenye eneo hilo. Watu wengine wanaoishi katika jengo hilo wamehamishwa. |
Polisi Ufaransa wamemzuilia mshukiwa
Posted by
RAMADHANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment