WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

A. Kusini waandamana kupinga ushuru

Vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini vimefanya maandamano kupinga viwango vipya vya ushuru wa barabara kati yaJohannesburgna mji mkuu Pretoria.
Mwandishi wa BBC mjiniJohannesburganasema maelfu wamejitokeza mitaani kwa mfano wa mikutano ya wakati ya kupinga ubaguzi wa rangi.
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Cosatu linasema utaratibu huo mpya utawaumiza wananchi.
Maandamano hayo pia yalielekezwa The protests are also directed against the practice of labour brokering - when agencies hire workers on short-term contracts.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Cosatu (Congress of South African Trade Unions) yanatokea katika miji 32 na majiji yote nchini Afrika Kusini.
Cosatu inasema inatrajia watu wapatao 100,000 wataunga mkono maandamano hayo.

Bahari ya wekundu

Mwandishi wa BBC Milton Nkosi mjiniJohannesburganasema mitaa ya mji huo imeenea rangi za shirikisho la Cosatu.
Ni moja ya maandamano makubwa kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni na inaonekanakamayale ya kupinga ubaguzi wa rangi wakati wa miaka ya 1980 na 1990, mwandishi wa BBC anasema.
Cosatu inatanua misuli yake, anaongeza, na kukionyesha chama tawala cha ANC kuwa ingawa kuna mikutano miwili shirikisho peke yake linafurahia kupata kuungwa mkono na wafanyakazi wa Afrika Kusini.
"Ushuru huo mpya utawaelemea mzigo maskini," Secretary General Zwelinzima Vavi aliwaambia waandishi kwenye maandamano hayo.
"Tunaiambia serikali, tuko tayari kwa mazungumzo. Mutuite tutakuja tukikimbia kutafuta," aliongeza.
Serikali ilirekebisha kiwango cha barabara kuu za ndani na kuzungukaJohannesburgkwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.
Inasema kazi hiyo haikuwa bure, na sasa inataka mfumo wa kieletronik wa kuchukua ushuru kuzigharamia ubora wake barabara zote na kuzipanua.
Kuanzishwa kwa ushuru huo tayari kulicheleweshwa mara kadhaa baada ya makampuni kuonya kuwa ushuru huo ungepandisha gharama za kuendesha huduma.
Cosatu pia inataka kuona kumalizika kwa matumizi ya wakala katika ajira ambayo inasema malipo kwa mawakala yanasababisha wafanyakazi kulipwa mishahara midogo na wanakosa marupurupu ya ajira zao.
Mwandishi wa BBC anasema Cosatu inakadiria watu milioni Afrika Kusini wameajiriwa kupitia mawakala


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: