WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Waandishi habari wauawa Syria

Serikali ya Ufaransa imethibitisha kwamba waandishi habari wawili wa kimataifa wameuawa katika mji wa Homs, Syria.
Msemaji wa serikali amesema waliokufa ni pamoja na Marie Colvin mwandishi wa kimataifa kutoka Marekani pamoja na mpiga picha raia wa Ufaransa Remi Ochlik. Bi Colin alikuwa mwandishi wa gazeti la Sunday Times huko Marekani.
Wanaharakati wa Syria wamesema wawili hao walikufa baada ya kombora kupiga nyumba walimokuwa wakipeperushia matangazo yao eneo la Baba Amr.
Kwenye ripoti yake hapo Jumanne Colvin alisema mashambulizi ya jeshi la serikali yalifanywa bila kujali usalama wa raia.
Mwanaharakati wa Syria ambaye amekuwa akitoa kanda za video pia aliuawa mjini Homs.


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: