WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Mitt Romney ameshinda katika jimbo la Nevada, kwenye mashindano ya kutafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican.
Mitt Romney na wafuasi wake Nevada

Juma lilopita alipata kura nyingi za wafuasi wa Republican katika jimbo la Florida.
Huku kura zinahisabiwa, tayari Bwana Romney alipata asili-mia-40 ya kura za wafuasi, na hivo kumshinda mpinzani wake, Newt Gingrich.
Akihutubia wafuasi wake kwenye mkutano mjini Las Vegas, Nevada, Bwana Romney alishambulia uongozi wa Rais Barack Obama:
"Rais Obama anaipa jina baya na kudharau karibu kila sekta ya uchumi wetu.
Lakini mimi ntaifanya Marekani ivutie sana wafanya biashara, wabunifu na wanaounda nafasi za ajira, ili Marekani ifanye kazi tena.
Na tofauti na watu wengine wanaogombea urais, kazi hiyo naijua vizuri."

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: