WELCOME TO THE REPUTABLE BLOG IN TOWN WITH FANTASTIC NEWS,GOSSIP,TALENTS,FASHION,MOVIE STAY ON THIS WEBSITE
RSS

Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za kibinadamu linatarajiwa kuandaa mazungumzo mengine ya dharura kuhusu Syria hivi leo , hii ikiwa ni punde tu baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya wachunguzi wa Umoja huo kuhusu kuenea kwa udhalimu dhidi ya raia. Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia haki za binadamu halina ushawishi mkubwa lakini linaweza kutumia uwezo wake wa kimaadili. Wajumbe wanaokusanyika mjini Geneva wanaonya kuwa watu wanaopaswa kuwajibikia ghasia za Syria lazima wakabiliane na mkono wa sheria. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alitoa wito wa Syria kushtakiwa katika mahakama ya kimataifa kuhusu jinai yaani ICC. Hata hivyo Urusi ilipinga kuanzishwa kwa mjadala mpya kwenye baraza hilo la haki za binadamu na huenda ikapiga kura kupinga uamuzi wowote ambao unaonekana kuidhalalisha serikali ta Syria. Baraza hilo linatarajiwa kutoa wito wa mashirika ya kutoa msaada kupewa nafasi ya kusafirisha na kusambaza msaada. Huku hayo yakiarifiwa shirika la Red Crescent limeweza kuokoa watu watatu kutoka wilaya ya Baba Amr huko Homs lakini halikufaulu kuchukua maiti za waandishi wawili wa habari waliouawa wiki iliopita au kuwaokoa waandishi wengine wawili waliojeruhiwa. Walio okolewa ni raia wa Syria ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja mja-mzito.

Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za kibinadamu linatarajiwa kuandaa mazungumzo mengine ya dharura kuhusu Syria hivi leo , hii ikiwa ni punde tu baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya wachunguzi wa Umoja huo kuhusu kuenea kwa udhalimu dhidi ya raia.
Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia haki za binadamu halina ushawishi mkubwa lakini linaweza kutumia uwezo wake wa kimaadili.
Wajumbe wanaokusanyika mjini Geneva wanaonya kuwa watu wanaopaswa kuwajibikia ghasia za Syria lazima wakabiliane na mkono wa sheria.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alitoa wito wa Syria kushtakiwa katika mahakama ya kimataifa kuhusu jinai yaani ICC.
Hata hivyo Urusi ilipinga kuanzishwa kwa mjadala mpya kwenye baraza hilo la haki za binadamu na huenda ikapiga kura kupinga uamuzi wowote ambao unaonekana kuidhalalisha serikali ta Syria. Baraza hilo linatarajiwa kutoa wito wa mashirika ya kutoa msaada kupewa nafasi ya kusafirisha na kusambaza msaada.
Huku hayo yakiarifiwa shirika la Red Crescent limeweza kuokoa watu watatu kutoka wilaya ya Baba Amr huko Homs lakini halikufaulu kuchukua maiti za waandishi wawili wa habari waliouawa wiki iliopita au kuwaokoa waandishi wengine wawili waliojeruhiwa.
Walio okolewa ni raia wa Syria ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja mja-mzito.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 maoni: